wapo wanaoamini kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 31 2010 , nchini Tanzania ulimpa ushindi aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbroad Slaa.
kwa mujibu wa habari zilizoandikwa katika gazeti la Tanzania Daima la tarehe 16 desemba 2010 , siku chache baada ya uchaguzi kumalizika zilisema "taarifa za kuaminika kutoka kwa vigogo wa usalama wa Taifa zinasema Dk Slaa aliekuwa akiwania kiti hicho kupitia CHADEMA alishinda uraisi kwa kuzoa asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa kwa nafsi hiyo lakini kwa makusudi matokeo halali yalichakachuliwa kumpa ushindi Jakaya Kikwete wa chama cha Mapinduzi (CCM).
"Mtoa taarifa wetu (Tanzania Daima) kutoka ndani ya idara hiyo amelithibitishia gazeti hili kuwa mbali na kujizolea asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa Dk slaa aliongoza kwa kupata kura nyingi kwenye mikoa 10 dhidi ya kikwete alieongoza kwa kura chache katika mikoa iliyosalia"
"Katika matokeo hayo yaliyovujishwa ndani ya siku tatu zilizopita inadaiwa kuwa kikwete alipata asilimia 27 tu ya kura zote zilizopigwa kwa nafasi hiyo ya urais huku asilimia 9 ya kura hizo ikienda kwa vyama vingine kikiwemo chama cha wananchi (CUF).
Taarifa hizo ziliendelea kuwa matokeo ya urais yalibadilishwa katika hatua ya ujumlishaji wa kura kwenye majimbo mbalimbali ambapo pale Dk Slaa alipoongoza kwa kura nyingi sana, kura hizo zilikuwa zikipunguzwa ili kukaribiana na zili za kikwete".
Mfano wa majimbo ambayo kura zake zilibadilishwa dakika za mwisho na tume ni Ubungo, Musoma mjini, Mbeya mjini, Arusha mjini, Ilala, kawe, Geita, Kilombero, Moshi mjini, Tarime na Songea mjini... hata hivyo Usalama wa Taifa walikanusha habari hizo. MWISHO WA KUNUKUU.Swali langu linakuja, kwanini chaguzi nyingi za Afrika zimekua zikitawaliwa na malalamiko na mizengwe ?...
ipo mifano mingi sana barani Afrika ambayo inaonesha hali ya utata wakati wa uchaguzi.
KENYA: 2007:katika Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 inaonesha chama cha aliyekua mgombea wa Orange Democratic Change (ODM), Bw. Raila Odinga alishinda katika Uchaguzi huo, kwa mujibu wa jumla ya kura kutoka katika vituo.
lakini taarifa zilisema tume ya uchaguzi Kenya, ilitumiwa kwa makusudi kubadlisha matokeo hayo, na kumpa ushindi Bw. Mwai Kibaki. hali hiyo ilisababisha machafuko nchini humo kupinga matokeo hayo, kiasi kilichopelekea watu 1000 kupoteza maisha yao, na wengine 500,000 zaidi kukimbia makazi yao.

ZIMBABWE: UCHAGUZI 2008: machi 29, uchaguzi wa zimbabwe ulifanyika.
Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, aling'ang'ania madaraka ili aendelea kuwa Rais kwa mara nyingine tena kwa kile kinachodaiwa kubadilisha matokeo ya uchaguzi, katika hatua ya pili, pale alipopata 85.5% ya kura zote dhidi ya 9.3% za Bw. Morgan Tsvangirai, taaarifa zilisema.
Bw. Morgan Tsvangirai aliyekua mgombea wa Movement for Democratic change (MDC), ilionesha ameshinda katika uchaguzi huo kwa hatua ya kwanza kwa kupata 47.9% ya kura zote dhidi ya 43.2% za Bw. Robert Mugabe.
lakini inadaiwa nguvu ilitumika kumbakisha Bw. Mugabe, kwa kile kinachodaiwa kuchakachua matoke ya hatua hiyo ya pili, na kumtangaza Mshindi wa uchaguzi huo. hali hii ilisababisha msukosuko wa uchumi katika nchi hiyo, hali iliyopelekea fedha yake kushuka thamani kwa kiasi kikubwa, na kuongeza ukali wa maisha kwa wananchi nchini humo.

COTED' VOIRE: 2010. Alassane Ouatarra, aliyekua kiongozi mkuu wa upinzani alishinda kihalali katika uchaguzi huo wa Coted' voire, tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo ilitangaza.
lakini chakushangazi Rais Laurent Gbagbo wa nchi hiyo, aliyeshindindwa katika uchaguzi huo alikataa kukabidhi madaraka kwa aliyeshinda. hali hiyo ilisababisha machafuko ya kisiasa nchini humo, na kusababisha wasiwasi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, dhidi ya majeshi yaliyokua yakimtii Bagbo na yale ya Quattara.

HIYO NI MIFANO MICHACHE TU.
zipo nchi nyingi za kiafrika zinazokutana na kile kinaachoitwa " ubabe wa viongozi waliopo madarakani.
swali langu: ni kwanini viongozi wengi hasa wa nchi za kiafrika hufanya "hujuma" wakati wa uchaguzi?
Je nikutaka kutunza heshima ya chama? ni kwa ajili ya maslahi binafsi? ni uoga ili kuendelea kuficha maovu? au ni kutumiwa na nchi za magharibi na Marekani n.k.... majibu yanaweza yakawa mengi sana.
mimi nadhani ifikie mahala, viongozi wetu wajue maana ya "demokrasia ya kweli" na waiheshimu pia. kunakua hakuna maana ya kufanya uchaguzi ilihali mtu anajua mwisho mshindi ni flani, eti kwasabu yeye ana nguvu ya ziada kwa kua anashikilia "dola".
viongozi wa Afrika wajifunze kuheshimu maamuzi ya wananchi. hii itasaidia kupunguza machafuko mengi ya kisiasa na kiuchumi pia, ambayo kwa kiasi kikubwa yamesabishwa na viongozi "walafi wa madaraka, wasiokuwa waaminifu na wanaojali maslahi binafsi".
lakini pia viongozi wa Afrika wajifunze kutoka kwa "Rupiah Banda, aliyekuwa Rais wa Zambia, ambaye hatimaye amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Nchini humo mapema mwezi septemba mwaka huu, NA KUAMUA KUHESHIMU "DEMOKRASIA" na maamuzi ya wapiga kura.
Taarifa zinasema" Rais wa Zambia Rupiah Banda amekubali kushindwa kwake na kiongozi wa upinzani Michael Sata. Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.
"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote
tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta
machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake. Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.
"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu,
tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna
nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.
Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.
Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.
Mwandishi wa BBC Louise Redvers kwenye mji mkuu, Lusaka, alisema kuhusu tangazo hilo, wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.
Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.
WITO WANGU KAMA MPIGA KURA.
Viongozi wetu wajifunze kuheshimu demokrasia ya Kweli hususani wakati wa uchaguzi, ili kuepusha migogoro ya kisiasa na machafuko ambayo yanaweza kutokea.
na waige mfano na funzo lililotolewa na Rupiah Banda na chama chake kwa kukabidhi madaraka pale waliposhindwa, kwa kufuata misingi ya Demokrasia ya kweli na utawala bora.
![]() |
| Bw. Rupiah Banda |

ni wakati muafaka wa nchi zingine za kiafrika, kuiga funzo lililotolewa na Zambia katika uchaguzi mkuu wa 2011.
ReplyDeleteAsiekubali kushindwa si mshindani..... wahenga walisema.