Mkuu wa usalama wa Kanali Gaddafi ni miongoni mwa maafisa kadhaa
washirika wake waliowasili katika mji mkuu wa Niger, Niamey, maafisa
wamesema.
____________________________________________________________________Wanasema mkuu huyo, Mansour Daw, aliingia nchini Niger Juamapili akiwa amesafiri kupitia njia ya jangwani karibu na mji wa Agadez.
Wakati huo huo, msafara uliotajwa kuwa na washirika wa karibu wanaomtii Kanali Gaddafi ukiwa na silaha nzito na fedha na dhahabu umeelekea katika mji mkuu wa Niger.
Maafisa wa Niger wanasema haiaminiki iwapo Kanali Gaddafi yuko pamoja nao.
Kamanda mwandamizi wa waasi alisema anaamini Kanali Gaddafi bado yuko Libya, lakini akiondoka kukimbia maeneo ambayo mapigano yanatokea.

No comments:
Post a Comment