Ferry iliyoelemewa uzito, iliyokua imebeba zaidi ya abiria 800, imezama katika bahari ya Hindi ikitoka Zanzibar kwenda kisiwa cha Pemba, huku mamia ya watu wakihofiwa kupotea.
Ferry hiyo, MV Spice Islanders ilikua imeelemewa uzito. taarifa kutoka Polisi kisiwani Zanzibar zinasema, kikosi cha uokoaji wameweza kuopoa miili 192, na kuwatoa wengine 606.
Abdullah Saied said mmoja wa walionusurika, na baadhi ya abiria waliokua wapande Ferry hiyo, walisema walikataa kupanda Ferry hiyo ilipokua ikiondoka bandarini.
Ferry hiyo imezama katika eneo lenye mawimbi makubwa, kwenye kina kirefu kati ya Tanzania Bara na kisiwa cha Pemba mnamo majira ya saa 7 mchana, siku ya Jumamosi.
"nilihisi kitu kisichokua cha kawaida katika mwenendo wa Meli. ilikua ni kama zig-zag au kuyumbayumba" alisema Yahya Hussein, mwenye miaka 15, ambaye alinusurika kwa kushikiria ubao mrefu pamoja na wenzie watatu.
"baada ya kugundua kuna dalili ya meli kuzama nikarukia upande wa juu wa meli, na baada ya muda mfupi meli ikaanza kuzama, aliongeza kijana Yahya Hussein.
__________________________________________________________________
__________________________________________________________________
Binti Hussein bin said alisema kulikua na watoto wengi ndani ya Meli.
karibu ya watu 260 wameripotiwa kuokolewa, huku watu 107 wakithibitishwa kufa maji.
Mohammed
Aboud Mohammed, waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais amesema miili 45 imeopolewa.baadhi ya watu wametoa maoni, huku wakionesha kukasirishwa na kitendo cha Meli hiyo kuruhusiwa kuondoka bandarini, na wakisisitiza maafisa wa serikali wajiuzulu.
wameendelea wakisema kua serikali ilitakiwa kuwa na waokoaji na boti za uokoaji, badala ya boti moja iliyopo inayotumika kudhibiti shughuli haramu majini, ambayo pia ni ndogo.
___________________________________________________________________
The Telegraph

No comments:
Post a Comment