Kurasa za maisha: blogs list

Monday, September 26, 2011

MAKALA: MARAIS WA AFRIKA NA TUHUMA ZA "HUJUMA" WAKATI WA UCHAGUZI.

wapo wanaoamini kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 31 2010 , nchini Tanzania ulimpa ushindi aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbroad Slaa.

kwa mujibu wa habari zilizoandikwa katika gazeti la Tanzania Daima la tarehe 16 desemba 2010 , siku chache baada ya uchaguzi kumalizika  zilisema  "taarifa za kuaminika kutoka kwa vigogo wa  usalama wa Taifa zinasema Dk Slaa aliekuwa akiwania kiti hicho kupitia CHADEMA alishinda uraisi kwa kuzoa asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa kwa nafsi hiyo lakini kwa makusudi matokeo halali yalichakachuliwa kumpa ushindi Jakaya Kikwete wa chama cha Mapinduzi (CCM). 

"Mtoa taarifa wetu (Tanzania Daima) kutoka ndani ya idara hiyo amelithibitishia gazeti hili kuwa mbali na kujizolea asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa Dk slaa aliongoza kwa kupata kura nyingi kwenye mikoa 10 dhidi ya kikwete alieongoza kwa kura chache katika mikoa iliyosalia"  

"Katika matokeo hayo yaliyovujishwa ndani ya siku tatu zilizopita inadaiwa kuwa kikwete alipata asilimia 27 tu ya kura zote zilizopigwa kwa nafasi hiyo ya urais huku asilimia 9 ya kura hizo ikienda kwa vyama vingine kikiwemo chama cha wananchi (CUF). 

Taarifa hizo ziliendelea kuwa matokeo ya urais yalibadilishwa katika hatua ya ujumlishaji wa kura kwenye majimbo mbalimbali ambapo pale Dk Slaa alipoongoza kwa kura nyingi sana,  kura hizo zilikuwa zikipunguzwa ili kukaribiana na zili za kikwete".  

Mfano wa majimbo ambayo kura zake zilibadilishwa dakika za mwisho na tume ni Ubungo, Musoma mjini, Mbeya mjini, Arusha mjini, Ilala, kawe, Geita, Kilombero, Moshi mjini, Tarime na Songea mjini... hata hivyo Usalama wa Taifa walikanusha habari hizo. MWISHO WA KUNUKUU.




Swali langu linakuja, kwanini chaguzi nyingi za Afrika zimekua zikitawaliwa na malalamiko na mizengwe ?...


ipo  mifano mingi sana barani Afrika ambayo inaonesha hali ya utata wakati wa uchaguzi.

KENYA: 2007:katika Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 inaonesha chama cha aliyekua mgombea wa Orange Democratic Change (ODM), Bw. Raila Odinga alishinda katika Uchaguzi huo, kwa mujibu wa jumla ya kura kutoka katika vituo.

lakini taarifa zilisema tume ya uchaguzi Kenya, ilitumiwa kwa makusudi kubadlisha matokeo hayo, na kumpa ushindi Bw. Mwai Kibaki.  hali hiyo ilisababisha machafuko nchini humo kupinga matokeo hayo, kiasi kilichopelekea watu 1000 kupoteza maisha yao, na wengine 500,000 zaidi kukimbia makazi yao. 



ZIMBABWE: UCHAGUZI 2008: machi 29, uchaguzi wa zimbabwe ulifanyika. 

Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, aling'ang'ania madaraka ili aendelea kuwa Rais kwa mara nyingine tena kwa kile kinachodaiwa kubadilisha matokeo ya uchaguzi, katika hatua ya pili, pale  alipopata 85.5% ya kura zote dhidi ya 9.3% za Bw. Morgan Tsvangirai, taaarifa zilisema. 

Bw. Morgan Tsvangirai aliyekua mgombea wa Movement for Democratic change (MDC),  ilionesha ameshinda katika uchaguzi huo kwa hatua  ya kwanza kwa kupata 47.9% ya kura zote dhidi ya 43.2% za Bw. Robert Mugabe. 

lakini inadaiwa nguvu ilitumika kumbakisha Bw. Mugabe, kwa kile kinachodaiwa kuchakachua matoke ya hatua hiyo ya pili, na kumtangaza Mshindi wa uchaguzi huo. hali hii ilisababisha msukosuko wa  uchumi katika nchi hiyo, hali iliyopelekea fedha yake kushuka thamani kwa kiasi kikubwa, na kuongeza  ukali wa maisha kwa wananchi nchini humo.



COTED' VOIRE: 2010. Alassane Ouatarra, aliyekua kiongozi mkuu wa upinzani alishinda kihalali katika uchaguzi huo wa Coted' voire, tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo ilitangaza. 

lakini chakushangazi Rais Laurent Gbagbo wa nchi hiyo, aliyeshindindwa katika uchaguzi huo alikataa kukabidhi madaraka kwa aliyeshinda. hali hiyo ilisababisha machafuko ya kisiasa nchini humo, na kusababisha wasiwasi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, dhidi ya majeshi yaliyokua yakimtii Bagbo na yale ya Quattara.


HIYO NI MIFANO MICHACHE TU.
zipo nchi nyingi za kiafrika zinazokutana na kile kinaachoitwa " ubabe wa viongozi waliopo madarakani.

swali langu:  ni kwanini viongozi wengi hasa wa nchi za kiafrika hufanya "hujuma" wakati wa uchaguzi?
Je nikutaka kutunza heshima ya chama? ni kwa ajili ya maslahi binafsi?  ni uoga ili kuendelea kuficha maovu? au ni kutumiwa na nchi za magharibi na Marekani n.k....  majibu yanaweza yakawa mengi sana.


mimi nadhani ifikie mahala, viongozi wetu wajue maana ya "demokrasia ya kweli" na waiheshimu pia. kunakua hakuna maana ya kufanya uchaguzi ilihali mtu anajua mwisho mshindi ni flani, eti kwasabu yeye ana nguvu  ya ziada kwa kua anashikilia "dola". 
viongozi wa Afrika wajifunze kuheshimu maamuzi ya wananchi. hii itasaidia kupunguza machafuko mengi ya kisiasa na kiuchumi pia, ambayo kwa kiasi kikubwa yamesabishwa na viongozi "walafi wa madaraka, wasiokuwa waaminifu na wanaojali maslahi binafsi".
lakini pia viongozi wa Afrika wajifunze kutoka kwa "Rupiah Banda, aliyekuwa Rais wa Zambia, ambaye hatimaye amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu  uliofanyika Nchini humo mapema mwezi septemba mwaka huu, NA KUAMUA KUHESHIMU "DEMOKRASIA" na maamuzi ya wapiga kura.
 
Taarifa zinasema" Rais wa Zambia Rupiah Banda amekubali kushindwa kwake na kiongozi wa upinzani Michael Sata.  Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.

"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake. Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.




Bw. Rupiah Banda
"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.


Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.


Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.


Mwandishi wa BBC Louise Redvers kwenye mji mkuu, Lusaka, alisema kuhusu tangazo hilo, wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.


Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.


WITO WANGU KAMA MPIGA KURA.


Viongozi wetu wajifunze kuheshimu demokrasia ya Kweli hususani wakati wa uchaguzi, ili kuepusha migogoro ya kisiasa na machafuko ambayo yanaweza kutokea. 

na waige mfano na funzo lililotolewa na  Rupiah Banda na chama chake kwa kukabidhi madaraka pale waliposhindwa, kwa kufuata misingi ya Demokrasia ya kweli na utawala bora.

Wednesday, September 21, 2011

VIGOGO WANAOSHUKIWA KUSABABISHA GHASIA 2007 KENYA WAFIKISHWA "THE HAGUE" TENA.

 NAIROBI, KENYA. 
________________
Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta, Mkuu wa utumishi wa Umma Francis    Muthaura na aliyekuwa mkuu wa polisi Jenerali Hussein Ali watafika mbele  ya mahakama ya kimataifa ya jinai iliyoko the Hague Uholanzi ICC.
________________________________________________

Uhuru Kenyatta

zaidi ya watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo za baada ya uchaguzi.

Viongozi hao wanatuhumiwa kupanga ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Zaidi ya watu 1,000 waliuawa na wengine 500,000 walilazimika kuhama makaazi yao.

Mahakama hiyo inaanza kupokea ushaidi kuthibitisha ikiwa watu hao watafunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita. Viongozi wanaofika mahakamani leo ni washirika wa karibu wa Rais Mwai Kibaki.

Ghasia zilizuka baada ya wafuasi wa Rais Mwai Kibaki kutuhumiwa kujaribu kuvuruga uchaguzi wa urais.

Ghasia hizo zilimalizika wakati Bw Kibaki na hasimu wake Raila Odinga kukubaliana kugawana madaraka, huku Raila Odinga akiwa Waziri Mkuu.

Kulingana na mwandishi wa Shrika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mjini the Hague Peter Musembi, mwendesha mashtaka Louis Moreno Ocampo atawasilisha ushaidi wa watu kumi ambao wanasema Bw Kenyatta na Bw Muthaura walipanga mikutano na kundi haramu la Mungiki ilikuandaa mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Naibu Waziri Mkuu, ameamua kutoa ushaidi wake mwenyewe na atahojiwa na mawakili wa pande zote.

Kwa upande wake mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na aliyekuwa kamishna wa polisi wanapinga kesi hiyo dhidi yao kwa misingi kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuwafungulia mashataka.

William Ruto

Waziri wa zamani wa Elimu ya juu Wiliam Ruto, waziri wa zamani wa Viwanda Henry Kosgey na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang ni washukiwa wengine ambao walihusishwa na chama cha waziri mkuu Raila Odinga.


Washukiwa hao walifika mahakamani mapema mwezi huu kujibu mashtaka ya kupanga ghasia hizo na kusababisha maafa hayo.

_____________________________________________________________
Reuters/BBC




Saturday, September 17, 2011

Join Kurasa za Maisha for FREE and receive News Updates continuously!!!!

TODAY!!!!!!! KURASA ZA MAISHA officially begins to "blog" with various News updates!!!!!!!!!

EAST AFRICA - TANZANIA - DAR ES SALAAM - KINONDONI - VIJANA

(SEMINAR ON ONLINE  ENTERPRENEURSHIP!!!!!! By Mr. Mark Urio (Bcom - Finance (Hons - UDSM, MIB-International Business Dublin - U.K)     4:00 - 6:00 am

call: +255 765 669 603, Email: bmakeja@live.com. close at: 2:00 am

NOTICE!!!!!!!!!!!!!!









Friday, September 16, 2011

MAKALA: CLEOPATRA, MALIKIA ALIEPOTEZA DIRA YA MISRI.

Malkia Cleopatra ni maarufu zaidi kati ya malkia wote waliowahi kutawala Misri. 


Cleopatra alizaliwa Alexandria mwaka wa 69 K.K (kabla ya kristo),Wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII. Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa . Cleopatra hakua Mmisri, ispokuwa mMacedonia familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander  the Great. 


Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.
URITHI WA UTAWALA WA PTOLEMY

Mfalme wa Misri ,Ptolemy wa XII ,anakufa mnamo mwaka wa 51 K.K. anaacha utawala kwa kijana wake mdogo mwenye miaka  12 Ptolemy XIII.  Lakini anaagiza kwamba, kijana huyu atawale pamoja na dada yake mkubwa, Cleopatra.  Pia ni lazima amuoe, kama desturi ya utawala wa ukoo wa Ptolemy, ingawa ndoa hiyo ilikua ni kama kuigiza.

ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.
Cleopatra mwenye miaka 18 mapema anathibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususani katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania. Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.

Caesar na Cleopatra: 48-44 K.K


Kuwasili kwa Julius Caesar Alexandria, kunampa fursa Cleopatra kuonekana Ulimwenguni ,kwa wakati huo. Anaachia Misri, mikononi mwa  Julius Caesar ambaye baada ya kushinda vita Pompey anakua mtawala mwenye nguvu katika  dola ya Roma. 

Julius Caesar anaamua kupumzika  kati ya 47 – 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyu hata kuangamiza majeshi ya kaka yake  (ambaye hakuweza kufua dafu). 
Mara baada ya Caesar kuondoka Alexandria , Cleopatra anajifungua katika majira ya Kiangazi mnamo mwaka wa 47 K.K, anadai kuwa mtoto ni  wa Caesar, na pia anamfanana sana . 

Katika mwaka wa 46 K.K Caesar anamualika Cleopatra Roma pamoja na mwanae (ambae mara baada ya kuzaliwa alipachikwa jina  Caesarion, “Caesar mdogo) ambao walikaribishwa katika  jumba la kifahari likiwa na kila aina ya anasa. baadae caesar anauwawa.


Baada ya Caesar kuuwawa mwaka wa 44, Cleopatra aliamua kurudi Misri na mwanae.

ANTONIUS  NA CLEOPATRA, 41- 31 K.K

Misri ya Cleopatra bado ni utawala ambao ni huru. Lakini karibu kila sehemu ya ukanda wa Mediterrania unajihusisha na siasa za Roma na kuna uvumi umeenea Roma  kwamba Cleopatra  amemsaidia “Cassius, mmoja kati ya waliomuua Caesar.

Katika majira ya kipupwe mnamo mwaka  wa 41, Marcus Antonius anaamuru  majeshi ya Roma kwenda upande wa Mashariki, na anaamuru Cleopatra aje aeleze juu ya tuhuma dhidi yake katika makao makuu yake huko Anatolia. 


Cleopatra anavuka medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana simanzi.
Kambi ya Antonius iko Tarsus, maili kadhaa kwenda mto Cydnus. Malkia anawasili akiwa katika Boti ya kifahari , akiwa amevaa mavazi yakuvutia ya mahaba , yenye asili ya Kigiriki. Hazuiliki kutamanika, na mapenzi yake mara yanaangukia ndani ya nyumba ya jenerali Marcus Antonius. 


Cleopatra anamualika Antonius amtembelee Alexandria.

Anakubali mwaliko wake kwenda Misri kumtembelea, na anawasili Alexandria wakati muafaka kwa ajili ya kupumzika wakati wa majira ya Baridi. 

Baada ya Antonius  kuondoka kurudi Roma, Cleopatra patra anajifungua mapacha, mvulana na msichana. Wanakaa muda mrefu, hadi mwaka wa 37 K.K ndipo Cleopatra na wanawe wanaungana tena na Antonius. 

Antonius Anamuagiza kuja Antioch, Syria ambako huko anamuoa.

Sasa wanajionesha waziwazi pamoja. na wanaungana kumpinga Octavian, mpinzani mkubwa wa Antonius katika Roma. 

Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki ,  anakua na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa mashariki ya kati (Syria).

Katika desturi ya tawala nyingi za Mashariki, Cleopatra na Antonius sasa wanakua na uwezo wa kuabudu katika miungu mmoja. Katika Ugiriki wanakua “Dionysus (Antonius) na Aphrodite (Cleopatra), katika desturi za wamisri wanakua Osiris na Isis, hali kadhalika.

Makutano katika  Alexandria 44 K.K

Makutano wengi wanakusanyika katika Alexandria, macho yao yakiangalia yanayojili toka kwa utawala huu, Katika jukwaa kuu ameketi Antonius na Mkewe Cleopatra akiwa amevaa mavazi ya sherehe maalum mithili ya miungu wa kike wa Misri. 

Na katika viti vingine  vinne vya kifalme wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na “Caesar –mdogo”, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.
Mnamo  majira ya jioni katika tafrija hii, ambayo baadae ilijulikana kama  “harambee katika Alexandria”, Antonius anaugawa utawala wa Medditerania Mashariki kwa familia yake hiyo mpya. 

Antonius anamtangaza Cleopatra kuwa “Malkia wa Wafalme, na “Caesar-mdogo kuwa Mfalme wa Wafalme, kwa pamoja wakitawala Misri na Cyprus. na tawala zingine kwa watoto wao. Kwa Alexander, kijana wake mkubwa (umri miaka 6), anampa sehemu ya mashariki mwa Euphratia; kwa Mapacha, dada zake Alexander, Cleopatra, anawapa Libya na Tunisia, na kwa kijana wake mdogo,  Ptolemy Philadelphus (miaka 2) ambaye amevaa mavazi ya kihistoria ya Macedonia, anamgawia Syria na sehemu kubwa ya Anatolia.
Inakua sherehe inayovutia, lakini ambayo baadae italeta uhasama na vita.

Actium na baadaye:  31-30 K.K

Mapigano kati ya majeshi ya Octavianus na yale ya Antonius na Cleopatra yanafanyika Actium, Ugiriki katika mwezi September. Pande zote mbili, wana majeshi makubwa ya miguu na  yale ya farasi, lakini pia swala jingine ni meli za kivita za Roma, waliokuwa nazo pia.

Antonius na Cleopatra wanafaida ya kuwa na meli 500, 100 zaidi ya zile za Octavianus ambazo ni 400. Hizi ni zana za mbao ambazo ni imara sana. Zikiongozwa na na jeshi mahiri linalofikia askari hadi  ya 250. Antonius anapanga jeshi lake la meli, pamoja na Cleopatra na majeshi yake nyuma, hazina kubwa ya Misri, tayari kwa mapigano. 

Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki. 

Katika mapigano ya Actium meli za Octavianus zilishinda;
Katika hatua flani, Antonius anamjulisha Cleopatra juu ya meli zake , na mpango wakuvunja mapigano na kutoroka nae. 

Antonius na Cleopatra wanafanikiwa kurudi, katika milki ya Cleopatra. Lakini wote wanaamua kujinyonga katika mwaka unaofuata, wakati Octavianus alipowasili Misri na jeshi lake. Marcus Antonius anaamua kujiua, malkia alijaribu kumshawishi kutofanya hivyo, lakini ilishindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuoneshwa kama mfungwa mbele ya halaiki. Hapa aliamua kufa tar. 12 Agosti 30 KK. 

“asp” nyoka aliemuu Cleopatra 30 K.K
Cleopatra anaamua kujiua , kama ishara ya ushujaa mkubwa. Mara nyingi alichukulia “serious” uwajibikaji wake kwa Misri. Na pia ndiyo mtawala pekee wa kutoka ukoo wake aliejifunza na kujua kuongea lugha ya Misri. 
Malikia anatambua kama akiwa hai tayari atakua mfungwa wa Octavianus.
Akilindwa na askari wake wachache katika sehemu ndogo ya makazi yake, anaagiza sumu ndogo ya nyoka, asp, ambayo inaingizwa kwa siri kupitia kwenye kikapu chake anachotumia kuletewa matunda.


Cleopatra anavaa mavazi yake mazuri ya ki-malikia, na analala katika kiti chake cha dhahabu. anamweka “asp” katika maziwa yake. Akijitoa kafara kwa “Amen-Re” mungu wa jua wa Misri. 

Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (asp).
Muda wa mwisho wa uhai wa Malkia unakua kama “maigizo”, na  unakumbukwa sana katika historia ya maisha yake. Na pia unaweka kikomo cha utawala wa Ptolemy katika Misri.

Octavianus alimtafuta pia Caesarion kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake, akamuua. Akawachukua watoto wote watatu wa Marcus Antonius, akawaonesha mbele ya halaiki ya Roma kuonesha ushindi wake. 
Pia anaichukua Misri kuwa sehemu ya utawala wa Roma, na kuchukua milki zote za ufalme wa Misri.


                                                     
                                                           
                            (c) Ben Makeja Jr. 2011

Monday, September 12, 2011

MLIPUKO WA MOTO WAUA ZAIDI 100 NAIROBI

Zaidi ya watu 100 wamekufa kwa  mlipuko wa moto uliosababishwa na kupasuka kwa bomba la mafuta, katika eneo la viwanda  jijini Nairobi Kenya, polisi wamesema.

Mlipuko huo umetokea katika eneo la viwandani la Lunga Lunga na askari wa zima moto walipambana na moto mkali ambao ulikuwa ukitishia makazi ya watu mjini humo.

Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja wa ndege.

Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali, maafisa wanasema.



Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema waathirika wengi waliungua kiasi cha kutokufatambulika.
Taarifa zinasema mlipuko huo huenda umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji ambao ulikuwa ukielea mafuta.

Mafuta hayo yalivuja kutoka kwenye tangi moja katika ghala linalomilikiwa na Kampuni ya Mafuta ya Kenya, msemaji wa polisi Charles Owino ameliambia shirika la habari la Uingereza (Reuters)
 
____________________________________
____________________________________

TAARIFA ZAIDI ZINASEMA:  

Polisi na jeshi wameweka vizuizi katika eneo hilo, ambapo wakazi walisema kuvuja kwa mafuta kwenye bomba hilo na kusababisha watu wengi kukimbilia kuchota mafuta yaliyovuja.

"Kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko, mlipuko mkubwa, na moshi na moto ukiwaka juu angani," mkazi mmoja Joseph Mwego aliliambia shirika la habari la AFP.

Sehemu ya miili ilionekana ikiungua kiasi cha mita 300 (futi 1,000) karibu na eneo la tukio, wenyeji walisema.

Miili mingine likuwa inaelea katika mto karibu na eneo hilo ambapo watu walioungua iliripotiwa waliruka baada ya kushika moto.
 
Vibanda vilivyoezekwa kwa mabati vimejengwa karibu kabisa na bomba hilo, wakazi walisema.

Kumekuwa na vifo vingine ambavyo vimetokana na watu kuchota mafuta yanayovuja: Zaidi ya watu mia moja walikufa eneo la Molo, magharibi mwa Kenya mwaka 2009 baada ya lori la mafuta kupinduka na moto kulipuka.

Sunday, September 11, 2011

HABARI KAMILI: karibu watu 200 Wahofiwa kufa Maji Zanzibar

Ferry iliyoelemewa uzito, iliyokua imebeba zaidi ya abiria 800, imezama katika bahari ya Hindi ikitoka Zanzibar kwenda kisiwa cha Pemba, huku mamia ya watu wakihofiwa kupotea.





Ferry hiyo, MV  Spice Islanders ilikua imeelemewa uzito. taarifa kutoka Polisi kisiwani Zanzibar zinasema, kikosi cha uokoaji wameweza kuopoa miili 192, na kuwatoa wengine 606.

Abdullah Saied said mmoja wa walionusurika, na baadhi ya abiria waliokua wapande Ferry hiyo, walisema walikataa kupanda Ferry hiyo ilipokua ikiondoka bandarini. 

Ferry hiyo imezama katika eneo lenye mawimbi makubwa, kwenye kina kirefu kati ya Tanzania Bara na kisiwa cha  Pemba mnamo majira ya saa 7 mchana, siku ya Jumamosi.

"nilihisi kitu kisichokua cha kawaida katika mwenendo wa Meli. ilikua ni kama zig-zag au kuyumbayumba" alisema Yahya Hussein, mwenye miaka 15, ambaye alinusurika kwa kushikiria ubao mrefu pamoja na wenzie watatu. 

"baada ya kugundua kuna dalili ya meli kuzama nikarukia upande wa juu wa meli, na baada ya muda mfupi meli ikaanza kuzama, aliongeza kijana Yahya Hussein. 
__________________________________________________________________

__________________________________________________________________

Binti Hussein bin said alisema kulikua na watoto wengi ndani ya Meli.

karibu ya watu 260 wameripotiwa kuokolewa, huku watu 107 wakithibitishwa kufa maji.          
Mohammed Aboud Mohammed, waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais amesema miili 45 imeopolewa.

baadhi ya watu wametoa maoni, huku wakionesha kukasirishwa na kitendo cha Meli hiyo kuruhusiwa  kuondoka bandarini, na wakisisitiza maafisa wa serikali wajiuzulu.

wameendelea wakisema kua serikali  ilitakiwa kuwa na waokoaji na boti za uokoaji, badala ya boti moja  iliyopo inayotumika kudhibiti shughuli haramu majini, ambayo pia ni ndogo.
___________________________________________________________________
The Telegraph















Saturday, September 10, 2011

BREAKING NEWS: AJALI YA MELI ZANZIBAR

Ferry iliyobeba abiria zaidi ya 500 kutoka Zanzibar kwenda kisiwa cha Pemba imezama, watu zaidi  ya 350 WAHOFIWA KUPOTEA.

TAARIFA ZINASEMA:  FERRY ILIKUWA NA ABIRIA  ZAIDI YA  500. kamishina wa Polisi zanzibar Said Mussa Ali Mussa, amethibitisha. watu wanaokadiriwa kufikia 260 wameokolewa , idadi ya watu waliofariki bado haijathibitishwa.

Taarifa kutoka kwa Kamishina pia zinasema: kikosi cha uokoaji kipo kinafanya kazi nzuri, kwa kusaidiana na boti kadhaa za uvuvi. 

MUNGU 

IBARIKI ZANZIBAR,

MUNGU 

IBARIKI TANZANIA.


HATIMAE FEDHA ZA RADA KULIPWA NA KAMPUNI YA "BAE SYSTEMS"

Kampuni ya kutengeneza silaha za kijeshi ya Uingereza BAE Systems, hatimaye imekubali kuilipa moja kwa moja serikali ya Tanzania dola milioni 47.
________________________________________________________________

Fedha hizo ni malipo ya ziada yaliyotokana na mauzo ya Rada ambayo yalikuwa ni zaidi ya fedha halisi ya ununuzi wa rada hiyo .
Uamuzi huo unahitimisha mvutano wa muda mrefu kuhusu ununuzi wa rada hiyo ambao ulifanyika katika mazingira ya rushwa na kusababisha mahakama nchini Uingereza kuamuru fedha hizo zirejeshwe Tanzania
Kampuni ya BAE Systems ilishutumiwa na wabunge wa Uingereza kwa kujivuta kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa zaidi ya mwaka mmoja uliopita .



Serikali ya Uingereza ilisema imeiambia BAE kuwa hawana budi kulipa malipo hayo na kutarajia kuwa suala hilo lingefikiwa muafaka kwa faida ya watanzania.
Awali katika taarifa yake rasmi BAE ilisema inafanya kazi na serikali ya Uingereza kupitia wizara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) kutoa malipo hayo kulingana na utaratibu wao.


BAE haikuwa tayari kuilipa serikali ya Tanzania fedha hizo na ilitaka ilipe kupitia misaada yake kwa mashirika ya hisani ya Uingereza yanayofanya kazi nchini Tanzania.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC (Idhaa ya Kiswahili) kutoka Kongwa Dodoma, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alisema ‘huku Tanzania tumeupokea uamuzi huo kwa furaha kubwa sana sana sana, kwa sababu ni jambo ambalo kwa upande wetu tukuwa tunaona kuwa si haki na kwa kuwa sasa fedha hizo zinarudi Tanzania, ‘Ni matumaini yetu kuwa fedha hizi zitatumika vizuri, kupitia serikali yetu kwa manufaa ya watanzania wote kama ilivyokusudiwa.’ Aliongeza Bw Ndugai.

Naibu Spika Job Ndugai miezi michache iliyopita aliongoza ujumbe wa wabunge wa Tanzania mjini London kufuatilia malipo hayo, baada ya kutokea mvutano wa muda mrefu kati ya serikali Tanzania na kampuni hiyo ya BAE.

Friday, September 9, 2011

TRENDS AMONG THE WORLD'S POOREST COUNTRIES

United Nations
Brethren,

Since 1970, there has been encouraging news emerging from developing countries. According to the UN's 2010 Human Development Report, life expectancy in developing countries has increased from 59 years in 1970 to 70 years in 2010. School enrollment climbed from 55% to 70% of all primary and secondary school-age children. Also, in the last forty years, per capita GDP doubled to more than ten thousand U.S. dollars.


The World's average Human Development Index (HDI), which combines information on life expectancy, schooling and income, has increased 19% since 1990 (and 41% since 1970). This reflects large improvements in life expectancy, school enrollment, literacy, and income. Almost every country has benefited from this progress. Only three countries have a lower HDI in 2010 than in 1970. Those three countries are Zimbabwe, Zambia, and the Democratic Republic of the Congo. Poor countries are catching up with the wealthier countries, but not all countries made fast progress. For example, the countries in Sub-Saharan Africa have progressed slowly, largely due to the HIV epidemic. Countries in the former Soviet Union have been held back by an increase in adult mortality.


1. Zimbabwe       
                                                                                            22. Tanzania (United Republic of)
2. Congo (Democratic Republic of the)
                                                                                            23. Djibouti
3. Niger
                                                                                            24. Angola
4. Burundi
                                                                                            25. Haiti
5. Mozambique
                                                                                            26. Senegal
6. Guinea-Bissau
                                                                                            27. Uganda
7. Chad
                                                                                            28. Nigeria
8. Liberia
                                                                                            29. Lesotho
9. Burkina Faso
                                                                                            30. Comoros
10. Mali
                                                                                            31. Togo
11. Central African Republic
                                                                                            32. Nepal
12. Sierra Leone
                                                                                            33. Papua New Guinea
13. Ethiopia
                                                                                            34. Mauritania
14. Guinea
                                                                                            35. Madagascar
15. Afghanistan
                                                                                             36. Benin
16. Sudan
                                                                                             37. Yemen
17. Malawi
                                                                                             38. Myanmar
18. Rwanda
                                                                                             39. Cameroon
19. Gambia
                                                                                             40. Ghana
20. Zambia
                                                                                             41. Bangladesh
21. Côte d'lvoire
                                                                                             42. Kenya


To illustrate the income inequality between rich and poor countries, consider these facts: about 1.75 billion people live in multi-dimensional poverty, meaning extreme deprivation in education, health, and standard of living; 1.44 billion people out of the developing world's 6.9 billion people live on $1.25 per day; 2.6 billion people are estimated to be living on less than $2 a day. Multidimensional poverty varies by region from three percent in Europe and Central Asia to 65% in Sub-Saharan Africa

NOTE: the later the number, the more the country has developed.
________________________________________
Source: Human Development Report (U.N 2010)






Wednesday, September 7, 2011

MAAFISA WA USALAMA WA GADDAFI WAWASILI NIGER

Mkuu wa usalama wa Kanali Gaddafi ni miongoni mwa maafisa kadhaa washirika wake waliowasili katika mji mkuu wa Niger, Niamey, maafisa wamesema.
____________________________________________________________________




Wanasema mkuu huyo, Mansour Daw, aliingia nchini Niger Juamapili akiwa amesafiri kupitia njia ya jangwani karibu na mji wa Agadez.


Wakati huo huo, msafara uliotajwa kuwa na washirika wa karibu wanaomtii Kanali Gaddafi ukiwa na silaha nzito na fedha na dhahabu umeelekea katika mji mkuu wa Niger.


Maafisa wa Niger wanasema haiaminiki iwapo Kanali Gaddafi yuko pamoja nao.

Kamanda mwandamizi wa waasi alisema anaamini Kanali Gaddafi bado yuko Libya, lakini akiondoka kukimbia maeneo ambayo mapigano yanatokea.

UHUSIANO WA LIBYA NA UINGEREZA WATIA SHAKA

                                            The U.K Prime Minister David cameron


Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema uchunguzi utaanza dhidi ya tuhuma kwamba majajusi wa Uingereza walihusika na mateso dhidi ya wafungwa katika jela wakati kanali Muammar Gadafi alipokuwa madarakani.
 __________________________________________________________________

Bwana Cameron amesema ni muhimu kwa uchunguzi huo kuangazia madai kwamba kulikuwa na uhusiano wa karibu kati ya maafisa wa upelelezi wa Uingereza na Libya hasa baada ya shambulizi la septemba kumi na moja.


Kulingana la stakabadhi zilizofichuliwa mjini Tripoli hivi majuzi, inadaiwa kuwa huduma za ujasusi nchini Uingereza huenda zilitumiwa kuwahamisha washukiwa wawili wa ugaidi hadi nchini Libya mnamo mwaka 2004.

Akizungumza katika Bunge, Bwana Cameron alisema madai hayo sasa yatachunguzwa pamoja na madai mengine kuwa Serikali ya Uingereza iliyopita iliruhusu uhusiano wake na Libya kuwa karibu kupita kiasi. Lakini hata hivyo Waziri Mkuu alitahadharisha kuwa watu hawapaswi kuharakisha kulaumu huduma za kijasusio za Uingereza.

Akizungumza dakika chache tu baadaye katika Bunge la Commons, Waziri wa Mashauri ya Kigeni katika Serikali iliyopita ya Labour, Jack Straw, alikariri madai ambayo yamerudiwa mara kadhaa sasa kuwa yeye na Mawaziri wengine walipinga mateso ya washukiwa walipokuwa mamlakani.

VOTE FOR MOUNT KILIMANJARO

Vote now by telephone for Mount Kilimanjaro to become among the New7Wonders of Nature

from Tanzania, at any time!
You can now vote using the new international telephone voting line, available 24 hours a day, for you to call and vote at any time, from any international telephone line anywhere in the world.
____________________________________________________________

How to vote by telephone in three easy steps:

  1. Dial one of these international telephone numbers:
    +1 869 760 5990
    +1 649 339 8080
    +44 758 900 1290
  2. At the end of the message, after the tone, insert the 4 digit code for your chosen nomine
  3. When you hear the thank you message, you are all done – you have voted by telephone !
  4. for Tanzania: details
Nominee code: 7716      
Nominee name:Kilimanjaro
Country:Tanzania