Kurasa za maisha: blogs list

Wednesday, September 21, 2011

VIGOGO WANAOSHUKIWA KUSABABISHA GHASIA 2007 KENYA WAFIKISHWA "THE HAGUE" TENA.

 NAIROBI, KENYA. 
________________
Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta, Mkuu wa utumishi wa Umma Francis    Muthaura na aliyekuwa mkuu wa polisi Jenerali Hussein Ali watafika mbele  ya mahakama ya kimataifa ya jinai iliyoko the Hague Uholanzi ICC.
________________________________________________

Uhuru Kenyatta

zaidi ya watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo za baada ya uchaguzi.

Viongozi hao wanatuhumiwa kupanga ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Zaidi ya watu 1,000 waliuawa na wengine 500,000 walilazimika kuhama makaazi yao.

Mahakama hiyo inaanza kupokea ushaidi kuthibitisha ikiwa watu hao watafunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kivita. Viongozi wanaofika mahakamani leo ni washirika wa karibu wa Rais Mwai Kibaki.

Ghasia zilizuka baada ya wafuasi wa Rais Mwai Kibaki kutuhumiwa kujaribu kuvuruga uchaguzi wa urais.

Ghasia hizo zilimalizika wakati Bw Kibaki na hasimu wake Raila Odinga kukubaliana kugawana madaraka, huku Raila Odinga akiwa Waziri Mkuu.

Kulingana na mwandishi wa Shrika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mjini the Hague Peter Musembi, mwendesha mashtaka Louis Moreno Ocampo atawasilisha ushaidi wa watu kumi ambao wanasema Bw Kenyatta na Bw Muthaura walipanga mikutano na kundi haramu la Mungiki ilikuandaa mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Naibu Waziri Mkuu, ameamua kutoa ushaidi wake mwenyewe na atahojiwa na mawakili wa pande zote.

Kwa upande wake mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na aliyekuwa kamishna wa polisi wanapinga kesi hiyo dhidi yao kwa misingi kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuwafungulia mashataka.

William Ruto

Waziri wa zamani wa Elimu ya juu Wiliam Ruto, waziri wa zamani wa Viwanda Henry Kosgey na mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang ni washukiwa wengine ambao walihusishwa na chama cha waziri mkuu Raila Odinga.


Washukiwa hao walifika mahakamani mapema mwezi huu kujibu mashtaka ya kupanga ghasia hizo na kusababisha maafa hayo.

_____________________________________________________________
Reuters/BBC




No comments:

Post a Comment